FLASH


Thursday, January 24, 2013

Ninasikitika sana kwa haya

NASIKITISHWA SANA NA HAYA YANAYOENDELEA


Ninasikitika sana kwa haya yanayoendelea hapa nchini na hasa katika siasa za mfumo wa vyama vingi. Leo hii, kila baya likitokea CHADEMA basi CCM inaambiwa imeanzisha au imewatumia watu kuvuruga hili au lile.
SLAA na KADI YA CCM
Nape Nnauye alisema "kuna viongozi waandamizi wa CHADEMA wana kadi za CCM na wengine wanazilipia ada", ila hakutaja majina, baadaye Slaa alijitokeza hadharani na kukiri kwamba anayo na ameitunza kwa kuwa ni mali yake na anaienzi, hakufanunua anaienzi kwa namna gani. Hapa nani anatatizo?
Hata baada ya RUFAA ya LEMA (Mb), Tundu Lissu (Mb) alijibu suala la kadi hiyo inayomilikiwa na Slaa bila haya wakati jambo lenyewe lilikuwa halisemwi vizuri, na mwishowe huko Mbeya Katibu wake wa Mkoa alijiuzulu baada ya kuwa mmojawapo ya wanachdema waliokuwa wakipinga jambo lile.
Tujiulize, hivi leo akijitokeza kiongozi mwingine ndani ya chama hicho na kusema anakadi ya CCM itakuwaje? Kwa mfano Zitto KAbwe (Mb) afanye hivyo, itakuwaje? Hatutalazimika kuamini kwamba ametumwa?
Kule Tanga na Mbeya ambako walionesha hali ya kumpinga Slaa wengi wao wamelaumiwa na kuitwa wasaliti, kati ya Slaa na hao wanaompinga nani ni wasaliti?

Hebu tujikumbushe tukio la pale viwanja vya Jangwani Dar es Salaam, siku ile ambapo CHADEMA walikuwa wanazindua kampeni ya M4C, walizifanya nini kadi za CCM? walizikanyaga kwa shangwe na kuumiza mioyo ya watanzania ambao ni wapenzi wa CCM, kama kadi zile hazikuwa na thamani kwao, kwa nini Katibu Mkuu wake ambaye ndiye mtendaji mkuu wa CHAMA aenzi kisichopendwa na wenzake?

Ninachofahamu mimi ni kwamba, uanachama wa mtu unakoma kwa mambo mengi kama vile kifo, kushindwa kulipa ada na kujiunga na chama Kingine cha siasa. Na sharti ni kwamba, unapojiunga na chama kingine, unapaswa kuikbidhi kadi ile kwa Chama kipya unachojiunga, nao watakuwa na jukumu la kuikabidhi kadi ile kwa Chama ambacho mtu yule amehama. na hivyo unaposema nimepata wanachama kadhaa toka kwako ushahidi unakuwepo.

Mwaka 2012, CHADEMA walijigamba sana kwamba wamepokea wanachama wengi toka CCM bila ushahidi ila tulikuwa tunawaona na kadi za CCM ambao zilikabidhiwa kwao na wale waliohama CCM. Leo CCM inapokea wanachama toka kwao (CHADEMA), Mnyika anasema CCM wametengeneza kadi za CHADEMA na kuzigawa na watu wao na kisha kusema kwamba wamepata wanachama toka CHADEMA. Tujiulize, je hawa wanachama wapya wanatoka maeneo ya mbali? Maana hapa mtaani sisi wenyewe tunafahamiana. CHADEMA waache sababu na waseme kweli daima na waipende Demokrasia ili wapate maendeleo.

Kwa mtazamo wangu mimi, napenda kukiri kwamba, sehemu kubwa ya viongozi waandamizi wa CHADEMA walitoka CCM au chama fulani na walishawahi kuwa viongozi huko (rejea historia ya Slaa, Zitto Kabwe, J. Mnyika, Marando, Prof. Baregu. Prof Safari na wengine). Mimi binafsi, naamini kiongozi mkweli na anayekipenda CHADEMA kwa dhati ambaye hajawahi kuwa kiongozi au mwanachama wa CCM au chama kingine ni Freeman Mbowe (Mb) pekee, Huyu anasifa ya pekee.

BAVICHA
Ndani ya chombo hiki, wote wanatumiana. Pili wanabaguana na hawaminiani. Hili ni tatizo kubwa maana mwisho wa siku hakutakuwa na jambo la pamoja.
Na ninampongeza sana Zitto kwa kitendo chake cha kukataa kuzungumzia suala la URAIS 2015. Bavicha wakae vizuri, wapendane, waheshimiane na kuaminiana kama UVCCM. maamuzi ya Vikao pia yaheshimiwe.

Katika kumfukuza Shonza, ni wazi kabisa Demokrasia haikufuatwa. Huwezi kumfukuza mtu uanachama nje ya vikao halali. CHADEMA haijamfukuza Shonza, BAVICHA wamepata wapi mamlaka? Tena, BAVICHA haitoi uanachama kwa mtu kama UVCCM ambao unapswa kujaza fomu ya kuomba na kisha unapewa kadi, na tena gharama ya kulipia ada ya UVCCM ni kubwa kuliko hata CCM yenyewe kwa mwaka. katika hili kuna kichekesho. Lakini hapa napenda kumshauri Shonza, kufuata taratibu za Chama chake na sio kusema kila kitu kwenye vyombo vya habari. Pia asiseme uwongo kama anavyofanya Slaa Dkt.

Mwisho, CHADEMA wanapaswa kujipanga, CCM ina nguvu sana tena sana, propaganda zao zitakuja kuwagharimu siku moja na kujikuta hawaaminiki. Maana Dkt. Slaa naye ni mzuri sana kwa kusema uwongo na anapenda sana kutoa amri. Hizi sio sifa za kiongozi bora.

Mungu Ibariki CCM. Mungu Ibariki Tanzania.


No comments:

Post a Comment