FLASH

Sunday, February 3, 2013

SAKATA LA MITAALA NA UBORA WA ELIMULowassa amuunga mkono Mbatia 

NI KUHUSU UBOVU WA MFUMO WA ELIMU,ASEMA WABUNGE WENGI WANATAKA MITAALA IANGALIWE UPYA

Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa, akimkabidhi cheti mwanafunzi bora, Danny Kitalika wakati wa mahafali ya 13 ya Kidato cha Sita Shule ya Sekondari ya Benjamin William Mkapa yaliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Shule hiyo, Maneno Mbegu. Picha na Venance Nestory 
Na Ibrahim Yamola  (email the author)

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ameunga mkono hoja binafsi ya Mbunge wa Kuteuliwa, James Mbatia kuhusu udhaifu wa elimu nchini akisema, kuna udhaifu mkubwa katika sekta hiyo.
Lowassa alisema hayo jana katika Mahafali ya 13 ya Kidato cha Sita ya Shule ya Sekondari Benjamini William Mkapa, jijini Dar es Salaam ambapo alieleza kuwa sekta ya elimu inahitaji kufanyiwa marekebisho ili kuweza kuzalisha wahitimu wenye tija kwa taifa.
”Kuna tatizo la hali ya elimu nchini, tushirikiane wazazi, jamii, wanasiasa na wataalamu, tuangalie jinsi ya kusaidia sekta ya elimu kwa maana tutasaidia watoto wa nchi yetu,”alisema Lowassa.
Katika mahafali hayo, Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli mkoani Arusha kupitia (CCM) aliwakabidhi vyeti jumla ya wahitimu 330, kati yao wavulana 263 na wasichana 67 .
“Wabunge wengi bungeni tunakubaliana kwamba ipo haja ya kutazama upya suala zima la mitalaa ya elimu katika nchi yetu kwani elimu iliyopo inawaandaa watafuta kazi na siyo wanaotaka kujiajiri,”alisema Lowassa.
Alisema kuwa kukiwa na mfumo mzuri wa elimu wenye kuwaandaa wahitimu walio na uwezo wa kujiajiri wenyewe na kutokutegemea kuajiriwa taifa litapiga hatua.
Alihamisi wiki hii, Mbatia aliwasilisha bungeni Hoja Binafsi kuhusu Udhaifu wa Elimu Tanzania, akitaka mfumo mzima unaosimamia elimu nchini ufumuliwe, hoja iliyogeuka ‘kaa la moto’ kwa Serikali.
Baada ya majadiliano marefu kuhusu kuundwa kwa kamati ya kuchunguza mitalaa, sera na mihutasari ya elimu, hoja mbalimbali zilitolewa, huku baadhi ya wabunge wakitaka Kamati ya Bunge, wengine wakitaka iundwe tume huru ya kufuatilia suala hilo.
Mjadala huo uliendelea juzi asubuhi kwa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk Shukuru Kawambwa kusimama na kutetea mfumo wa elimu uliopo na kusisitiza kuwa Serikali inayo mitalaa, kabla ya wabunge kuchangia na Mbatia kuhitimisha akitaka kuiondoa hoja yake hadi Serikali itakapowasilisha mitalaa hiyo ya elimu bungeni.
Hata hivyo, Naibu Spika, Job Ndugai alikataa pendekezo la Mbatia na kutumia kanuni za Bunge za kuipitisha hoja hiyo kwa kuwahoji wabunge.
Baada ya hoja hiyo kupitishwa kwa kuungwa mkono na wabunge wengi wa CCM, hali hiyo iliwaudhi wabunge wa upinzani, ambao waliamua kutoka nje ya ukumbi.
Baadaye walikubaliana kumshtaki Waziri Kawambwa kwenye Kamati ya Bunge ya Mamlaka ya Haki, Kinga na Madaraka ya Bunge, wakimtaka ajiuzulu kwa kulidanganya Bunge, ikishindikana watalipeleka suala hilo kwa mamlaka zilizomteua. 
(chanzo gazeti la mwananchi)

chama cha mapinduzi chaacha neema kubwa mkoani Kigoma

SERIKALI CHAMA CHA MAPINDUZI CCM CHAACHA NEEMA KUBWA ZA MAENDELEA HUKO KIGOMA.....NAOMBA TUZIDI KUSONGA MBELE WATANZANIA..
HOSPITAL
BARABARA
DARAJA LA MTO MALAGALASI
VIWANADA VIDOGOVIDO WA UJASILIAMALI..
SERIKALI CHAMA CHA MAPINDUZI CCM CHAACHA NEEMA KUBWA ZA MAENDELEA HUKO KIGOMA.....NAOMBA TUZIDI KUSONGA WATANZANIA..
HOSPITAL
BARABARA
DARAJA LA MTO MALAGALASI
VIWANADA VIDOGOVIDO WA UJASILIAMALI..

KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana amewaachia neema wakazi wa wilaya ya Kibondo mkoani Kigoma, baada ya kuchangisha zaidi ya sh. milioni 18 za ujenzi wa wodi ya wazazi katika hospitali ya wilaya hiyo, kwenye mkutano wake wa hadhara uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Ushirika mjini wilayani hapa.

Katika mkutano huo ambao ulikuwa unahitisha ziaya ya siku mbili wilayani humo, ikiwa ni sehemu ya sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, ambazo kilele chake ni Jumapili hii kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma, Kinana alianza harambee hiyo kwa kuchangia sh. milioni 10.

Baada ya mchango huo aliwachagiza viongozi wote waliokuwa jukwaa nao wakatoa michango yao, wakiwemo Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi CCM, Alhaj Abdallah Bulembo ambaye alitoa milioni 2.3 na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma, Dk. Amani Kaborou aliyechangia sh. milioni moja.

Pamoja na michango hiyo, Kinana alitoa ahadi kwamba baada ya ujenzi wa wodi kukamilika Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete atatoa vifaa vyote vinavyotakiwa kuwemo ikiwa ni pamoja na vitanda vya kujifungulia kina mama.

"Ndugu wananchi kwa niaba ya Mwenyekiti wetu wa Chama Rais Jakaya Kikwete naomba kuahidi kwa niaba yake kwamba, baada ya ujenzi wa wodi kukamilika atatoa vifaa vyote vihavyohitajika kuifanya wodi itoe huduma bora, na kwa hili nina uhakika hataniangusha atatoa", alisema Kinana.

Uchangishaji huo ulifuatiwa na malamiko ya wananchi na baadjhi ya viongozi kwenye mkutano huo uliofurika maelfu ya watu, ambao walisema, hadi sasa hospitali ya wilaya ya Kibondo ina chumba kimoja tu cha wodi ya wazazi ambacho kakikidhi mahitaji kiasi kwamba baadhi ya wanaokwenda kujifungua wanalala chini kwa kukosa vitanda.

"Ndugu Katibu Mkuu wa CCM, nikiwa kama mama na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wilaya ya Kibondo na diwani wa Kata ya Kibondo mjini naomba kuweka bayana kwamba hapa tuna tatizo kubwa wa wodi ya kinana mama, tuna chumba kimoja tu ambacho hakitoshi kiasi kwamba baadhi ya wanaenda kujifungua hulala chini", alisema Joyce Chuma.

Mapema kabla ya harambee hiyo, Kinana alifanya harambee nyingine kwa ajili ya kusaidia kwenda shule za sekondari watoto wanaofaulu huku wakiwa walezi au wazazi wao hawana uwezo wa kuwasomesha.

Ombi la kufanyika harambee hiyo lilitolewa na Mkuu wa wilaya ya Kibondo, Venance Mwamoto ambaye alisema kwenye mkutano huo kwamba kuna kiasi cha watoto kumi ambao wameshindwa kwenda shule kutokana na wazazi au walezi wao kutokuwa na uwezo.

Ili kuchagiza uchangiaji huo, Mwamoto alijitolea mbuzi aliyeletwa mkutanoni Kinana akampiga mnada ambapo kwanza alimnunua mbuzi huyo kwa sh. milioni 3 na kuwapatia wasanii wa muziki wabongo Fleva ambao walitumbuiza kwenye mkutano huo.

Pamoja na Kinana wachangiaji wengine walijitokeza na hadi mwisho wa mnada zilipatikana sh. milioni 6.6.
Ili kufanya uchangiaji huo uwe endelevu Kinana aliahidi kutoa sh. milioni tatu kila mwaka endapo Mkuu huyo wa wilaya atafungua mfuko maalum wa kuwsomesha watoto ambao wamefaulu lakini wazazi au walezi wao hawana uwezo.

Akizungumzia kero ya muda mrefu ya Barabara ya Nyakanazi-Kigoma kupitia wilaya za Kibondo na Kasulu mkoani Kigoma, Kinana alisema, barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami kama ilivyoahidiwa na Rais Jakaya Kikwete wakatin wa kampeni.

"Wananchi ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami lazima utafanyika kwa sababu ahadi hii ipo katika ilani ya CCM na ni ahadi ya Rais Jakaya Kikwete hivyo msiwe na shaka na hili, nitamkumbusha Rais wetu, Jakaya Kikwete na bila shaka atalipa mkipaumbele swala hili", alisema Kinana.

Rais Jakaya Kikwete alitaraajiwa kuwasili mjini Kigoma leo Februari 2, 2013 kwa ajili ya sherehe za miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Jumapili hii kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.

Rais Jakaya Kikwete anataraajiwa kuwasili mjini Kigoma leo Februari 2, 2013 kwa ajili ya sherehe za miaka 36 ya CCM zitakazofanyika Jumapili hii kwenye Uwanja wa Lake Tanganyika.