FLASH


Saturday, November 16, 2013

FUATILIA ZIARA YA CCM MKONI RUVUMA NA HAPA NI HITIMISHO LA ZIARA WILAYA YA TUNDURU

KINANA AMALIZA ZIARA YAKE WILAYA YA TUNDURU KWA MAFANIKIO

Saturday, November 16, 2013
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari ya kata ya Mgomba pamoja na walimu wao,Katibu Mkuu alitembelea shuleni hapo kuona utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya maabara .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisaidiana na fundi katika kukamilisha hatua za mwisho za upigaji lipu wa wa jengo la maabara la shule ya Sekondari ya kata ya Mgomba iliyopo wilayani Tunduru.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwa kwenye picha ya pamoja na wanafunzi wa kidato cha kwanza wa shule ya sekondari ya Mgomba wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akiangalia  shughuli za ubanguaji korosho katika kiwanda cha kubangua korosho wilayani Tunduru.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha kubangua korosho cha Tunduru ambao walimweleza Katibu wa NEC kuwa wanalipwa kwa wiki na inategemea na idadi ya kilo ulizobangua.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akipata maelezo kuoka kwa meneja wa kiwanda hicho Ndugu Shinoy jinsi kodi za vyama vya ushirika zinavyokuwa mzigo kwao na kushauri bora zilipwe kwa mkulima moja kwa moja.
 Pichani ni wafanyakazi wa kiwanda cha kubangua korosho wakiwa kazini katika Kiwanda cha kubangua korosho cha Tunduru mkoani Ruvuma .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na mjumbe wa NEC wa wilaya ya Tunduru Mzee Kalolo,tayari kwa ufunguzi wa ofisi ya CCM kata ya Jakika jimbo la Tunduru Kaskazini.
 Ofisi ya Kata ya Jakika jimbo la Tunduru Kaskazini ambayo imefunguliwa rasmi na Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Jakika wakati wa ufunguzi wa ofisi ya kata ya Jakika iliyopo jimbo la Tunduru Kaskazini.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiongoza wananchi wa kata ya Jakika kwenda kuwasha tanuri la kuchomea matofali.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki kuwasha moto katika matanuri ya kuchomea matofali katika kata ya Jakika jimbo la Tunduru Kaskazini.
 Wananchi wakimpa mikono Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kama ishara ya kumkaribisha katika kijiji cha Matemanga wilaya ya Tunduru.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana pamoja na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye wakiongoza wananch wa Matemanga kwenda kusaidia shughuli za ujenzi wa nyumba mbili za madaktari ambazo zinajengwa na Taasisi ya Rais Mstaafu Ndugu Benjamin Mkapa.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia wakazi wa kijiji cha Matemanga wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa salaam za pongezi kwa taasisi ya Rais Mstaafu Ndugu Benjamin William Mkapa kwa ujenzi wa nyumba mbili za kuishi madaktari katika kituo cha Afya cha Matemanga wilayani Tunduru.
 Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akitoa mkono wa shukrani kwa fundi Denis Ngaiza baada ya kutoa ushirikiano wa kutosha katika ujenzi wa nyumba za Madaktari wa kituo cha afya cha Matemanga.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kijiji cha Milonde kata ya Matemanga katika kituo cha Kihuma wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
 Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Thabit Mwambungu na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Ruvuma Oddo Mwisho wakipitia kwa makini mambo mbali mbali katika nyaraka muhimu za taasisi ya huduma ya ya kiroho na kibinadamu ya Kihuma iliyopo wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akipiga kinanda wakati wanakwaya wa kikundi cha Kihuma wakitumbuiza .
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiweka jiwe la msingi la ofisi ya kata ya Mlingoti Mashariki wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
 Sehemu ya umati uliohudhuria mkutano wa hadhara wa CCM katika viwanja vya Baraza la Eid wilayani Tunduru ambao Katibu Mkuu wa CCM Ndgu Abdulrahman Kinana alihutubia.
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia umati wa wakazi wa wilaya ya Tunduru waliojitokeza kwa wingi kwenye viwanja vya Baraza la Eid, Nape aliwaambia wana Tunduru ni jukumu letu kulinda amani ya nchi na kutaka watu wasikubali kupotoshwa katika mchakato wa kupata Katiba Mpya.
 Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma Ndugu Oddo Mwisho akihutubia wakazi wa Tunduru kabla ya kumkaribisha  Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana kuja kuhutubia.
 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia umati wa wananchi katika viwanja vya Baraza la Eid wilayani Tunduru ambapo aliwaeleza wananchi hao kuwa CCM ni chama cha kutetea haki za wakulima na wafanyakazi na kuwambia wananchi hao kuwa kila kilichoahidiwa kitatimizwa.
 Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Ndugu Thabit Mwambingu akihutubia wananchi wa Tunduru namna Serikali inavyofungua mkoa wa Ruvuma kwa kuongeza na kujenga barabara na kuongeza matumizi ya anga.
 Mbunge wa Tunduru Kaskazini Ndugu Ramo Matala akihutubia wakazi wa Tunduru na kuwaambia taratibu za kuuza zao la korosho kwa pesa taslimu pia namna anavyosaidia shule na wananchi wakawaida wakiwemo walemavu ambao alikabidhi baiskeli zao, vifaa vya michezo na kusaidia boda boda kupata leseni.
Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akimpa mkono wa pongezi Ndugu Rajabu Matawaka mara baada ya kumkabidhi baiskeli ya walemavu iliyotolewa na mbunge ,Mbunge wa jimbo hilo alitoa vitabu, vifaa vya michezo na madawati 150.

ZIARA YA CHAMA MIKOA YA KUSINI KWA UFUPI

KINANA AHUTUBIA VIJIJI VITATU TUNDURU KUSINI

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na wananchi wa kata ya Mbesa ,kijiji cha Mbesa wilayani Tunduru ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mkoa wa Ruvuma ambayo ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa.
Katibu wa NEC Itikadi na Unezi Nape Nnauye akitoa ufafanuzi kwa wananchi wa kata ya Mbesa, kijiji cha Mbesa juu ya mpango wa serikali katika kuhakikisha wananchi hao wanapata maji,Kushoto Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana akisoma kitabu kinachoonyesha Mbesa ipo kwenye mpango wa kupata maji.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akishirikiana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk Asha-Rose Migiro  kujenga daraja la mto Munjapu wilayani Tunduru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyeshwa jinsi barabara itakavyokuwa baada ya kukamilika kwa daraja la mto Munjapu,lililopo kijiji cha Mnemasi, Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya kuimarisha chama,kusimamia ilani ya uchaguzi ya CCM 2010 katika mkoa wa Ruvuma akiwa ameongozana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa kwenye kijiji cha Mchoteka kwa staili ya aina yake ya kukimbia mchaka mchaka mapaka kwenye miradi ya ujenzi wa madarasa,maabara na nyumba za walimu katika shule ya Sekondari ya Mchoteka wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akishiriki ujenzi wa moja ya nyumba za walimu wa shule ya Sekondari Mchoteka,wilayani Tunduru.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akishiriki uchimbaji wa msingi wa vyumba vya maabara ya shule ya sekondari Mchoteka wilayani Tunduru.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na umati wa wananchi wa kijiji cha Mchoteka wilayani Tunduru mkoani Ruvuma.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kijiji cha Mchoteka waliofurika kutaka kumsikiliza, Katibu Mkuu alikuwa na ratiba ya kuonana na kumsalimia balozi wa nyumba kumi lakini kwa namna wananchi walivyojaa ilibidi ahutubie wananchi kwanza kabla ya kuonana na Balozi wa nyumba kumi.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa KImataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mchoteka wilayani Tunduru.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akiwasalimia wananchi wa kijiji cha Mchoteka waliojitokeza kwa wingi kuja kuwapokea viongozi wao wa kitaifa.
Babu Akuilaya (Babu Mkuu) kama heshima aliyopewa na Machifu wa Mchoteka,Ndugu Abdulrahman Kinana akiongea na wananchi wa kijiji cha Mchoteka na kuwashukuru kwa heshima waliyompa.
Katibu Mkuu wa CCM Taifa Ndugu Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa wanachama wapya wa CCM ambapo zaidi ya wanachama 100 wamejiunga na CCM katika kata ya Mchoteka.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipata mapokezi mazuri wakati akiwasili katika kata ya Nalasi,kijiji cha Nalasi wilaya ya Tunduru.
Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk.Asha-Rose Migiro akiimba na akina mama wakazi wa kata ya Nalasi waliojitokeza kwa wingi kuupokea ugeni .
Umati wa wakazi wa Kijiji cha Nalasi ukiwa umejaa kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye yupo kwenye ziara katika mkoa wa Ruvuma.

 Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wananchi wa kataNalasi ,wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma ambao walijitokeza kwa wingi kumsikiliza .
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Mkina kijiji cha Mkina ,wilya ya Tunduru mkoa wa Ruvuma.
 Baadhi ya wananchi wakisikiliza hotuba za viongozi wao wa CCM Taifa wakiwa juu ya miti.
Sehemu ya wakazi wa kata ya Mkina wakisikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Katibu Mkuu yupo kwenye ziara ya mikoa ya Ruvuma na Mbeya.Wananchi hao wamemueleza Katibu Mkuu wa CCM kuwa hawapo tayari kuuza korosho kwa mkopo,pia hawapo tayari kupangiwa bei na wanunuzi, wananchi hao waliitupia lawama bodi ya korosho pamoja na vyama vya ushirikia kwani vimeonekana havina msaada kwa wakulima.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mkina wilayani Tunduru mkoani Ruvuma ,Katibu Mkuu aliahidi kushirikiana nao katika kuhakikisha tatizo la zao la Korosho linapatiwa ufumbuzi kwani ni zao pekee linaloweza kuinua uchumi wa eneo hilo.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akionyesha moja ya leseni za dereva wa Boda Boda ambazo zilitolewa baada ya madereva hao kupata mafunzo ya kuendesha na ya usalama barabarani yaliosimamiwa na mbunge wa Tunduru Kusini Mtutura Abdallah Mtutura.