YAH:SHUKRANI YA UFANIKISHAJI
MKUTANO WA WANACHAMA TAWI MAALUM MZUMBE TAREHE 14/02/2016
Ndugu wanachama wa
chama cha mapinduzi, nimatumaini yangu sote tu wazima wa afya kwa uwezo wake
muumba. Kama ambayo kichwa cha habari hii hapo juu kinavyojieleza ni kwamba
siku ya tarehe 14/02/2016 uongozi wa ccm tawi maalum chuo kikuu mzumbe morogoro
tulifanikiwa kuendesha mkutano wa tawi uliotukutanisha wanachama wa ccm tawi
maalum mzumbe pamoja na viongozi wa jumuiya zingine zilizo chini ya chama cha
mapinduzi ambazo ni jumuiya ya wazazi, jumuiya ya vijana wa ccm na umoja wa
wanawake Tanzania. Mkutano huu ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini kama
tujuavyo shughuli yoyote ni watu hivyo namaanisha ufanisi wa mkutano huu pia
ulitokana na ushiriki wa watu kwa hali na mali kwa kiasi kikubwa hivyo nawiwa
kutuma salamu zangu za shukrani kwa wote waliofanikisha mkutano huu ukafanyika.
Shukrani
za dhati kabisa zimwendee Mh, diwani wa kata ya mvomero Bi. Recho Kingu kwa
kukubali kuacha majukumu yake na kukubali kuja kuwa mgeni rasimi katika mkutano
huo mbali na kuwa mgeni rasimi Mh. Kingu
pia alishirikiana nasi kwa ukaribu mkubwa kuhakikisha mkutano huu unafanyika
kama ilivyokusudiwa.
Bila
kumusahau Mh. Murad mbunge wa jimbo la mvomero naye hakuwa nyuma katika kuhakikisha
mkutano huu unafanyika bila kuwa na kipingamizi chochote aidha tawi maalum
mzumbe tunathamini sana mchango wake na kwa niaba ya wanachama wote niseme
asante sana mh. Mbunge wetu kwa ushiriki wako katika kuwezesha mkutano huo
ukawa wa mafanikio.
Nichukue
fursa hii pia kuwashukru Ndugu Boniphace Maiga na Maliki Malupu kwa kujitolea
kutoa darasa la itikadi na hamasa kwa wajumbe waliohudhuria mkutano huo naamini
wajumbe walijifunza mengi kutoka kwa wazungumzaji pia walihamasika vilivyo.
Napenda
pia kumshukru rais wa serikali ya wanafunzi wa mzumbe Mh. Yona Habiye kwa
ushiriki wake wa hali na mali kuhakikisha mkutano wetu unafanikiwa. Lakini pia
niwashukru viongozi wa shirikisho mkoa wa morogoro wakiongozwa na comrade
Kimako kwa kuja kujumuika nasi na kutoa ufafanuzi kwa wajumbe juu ya changamoto
zinazotukabili kama wanachama wa shirikisho mkoa wa morogoro, bila kumusahau
ndugu Alferd Salwa rais mstaafu wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu mzumbe kwa
sapoti yake katika kufanikisha mkutano.
Mwisho
kabisa niwashukru viongozi wote wa tawi maalum chuo kikuu mzumbe kwa
ushirikiano wetu tumeonesha kwa vitendo dhana ya UMOJA NI USHINDI na niwashukru
pia wanachama wote waliojitokeaza kushiriki katika mkutano huo nizidi kuwaomba
kwamba tusiwe wazungumzaji tu bali tuwe watendaji ili tumusapoti Rais wetu Dr, John Magufuli katika kutimiza ahadi
zake kwa watanzania maana jukumu la kutekeleza ilana ya uchaguzi ya ccm
2015/2020 ni jukumu la kila mwana ccm kwa nafasi aliyo nayo katika jamii yake.
Asanteni
sana wanachama wote wa tawi maalum chuo kikuu mzumbe na wote tulioshiriki
katika mkutano huo.
“SASA
KAZI KUJENGA NCHI NA KUKIJENGA CHAMA CHETU”
#KIDUMU
CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na:-
Katibu
ccm tawi maalum chuo kikuu mzumbe
Gwodwin
Komba
15/02/2016
No comments:
Post a Comment