FLASH


Wednesday, April 17, 2013

KILOSA NA GAIRO KWA UFUPI

CCM YAWASHA MOTO LEO GAIRO,


KINANA
GAIRO, MOROGORO, Tanzania
Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo kinatarajiwa 'kuuteka' mji wa Gairo kitakapofanya mkutano mkubwa wa hadhara kuanzia saa kumi jioni katika mji huo.
Kulingana na shamrashamra na simulizi zilizvyotanda miongoni mwa wananchi katika maeneo mbalimbali hapa Gairo, mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya watu, kwa ajili ya kumshudia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana ambaye anakuwa Gairo kwa mara ya kwanza tangu kuteuliwa kwake kushika wadhafa huo.
Mbali na Kinana ambaye aliwasili jana jioni, akitokea Kilosa, viongozi wengine wanaotarajiwa kuwasha moto kwenye mkutano huo,ni Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Dk. Mohammed Seif Khatib.
Kabla ya mkutano huo Kinana na ujumbe wake wamepangiwa kufanya shughuli mbalimbali za ujenzi wa Chama na ukaguzi wa ilani ya CCM, ikiwa ni pamoja na Kinana kufanya kikao cha ndani na  mabalozi na viongozi wa Chama ngazi wa kata zioizopo karibu na makao makuu ya wiyala.
Kaim Katibu wa CCM mkoa wa Morogoro, Sixtus Mapunda amesema asubuhi hii kiwamba, baada ya mkutano wa ndani, Kinana atafanya shughuli ya kukagua uhai wa chama katika mashina na matawi katika maeneo mbalimbali wilayani hapa


CCM YAFUNIKA KILOSA, MAMIA WAJITOKEZA KUMSIKILIA KINANA

Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana (kulia) akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara leo jioni mjini Kilosa, mkoani Morogoro.
  Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaini cha kitabu cha wageni kwenye Shina  la wajasiriamali wakereketwa wa CCM la Dinima, Kilosa katika ya kuwasili mjini Kilosa mkoani Morogoro kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara leo Aprili 17, 2-13.
Vijana wakisahngilia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, wakati msafara huo ukitoka Ifakara kwenda Kilosa  leo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na wanachama wa CCM shila namba 15, tawi la CCM Mbuni B, Kilosa. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi. Alyevaa miwani (kulia) ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Dk. mhammed Seif Khatib.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nap Nnauye (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) wakati amekaa na wajumbe wa shina  namba  15, tawi la CCM Mbuni B.
Viongozi kuanzia ngazi za mashina wa CCM katika wilaya ya Kilosa, wakizungumza na Kinana kwenye ukumbi wa Comfort, wilayani humo 
Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohamed Sif Khatib akitazama mahidi yalivyostawi kwenye shamba la mkulima maarufu wa wilayani Kilosa

NAPE AWASHUKIA WANASIASA KANJANJA

Katibu Mkuu wa CCM Taifa ndugu Abdulrahaman Kinana akisalimiana na wanachama wa shina la Ulaya Mbuyuni mara tu baada ya kulifungua rasmi ,Kilosa.
Shina hilo ni moja kati ya mashine manne aliyofungua wilayani Kilosa.

Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa ndani na  Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Ndugu Abdulrahaman Kinana.

Wazee waasisi na wanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi wakimsikiliza Katibu Mkuu,kwenye mkutano wa ndani hapo Kilosa.

Katibu wa NEC,Oganizesheni, Dr. Mohamed Seif  Khatibu akisalimia wananchi wa Kilosa.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wananchi wa Kilosa na kuwapa pongezi kushiriki kwenye  mchakato wa Katiba  Mpya, na pia aliwagusia wananchi kuwa makini na makanjanja wa kisiasa.

Katibu Mkuu wa CCM akihutubia wananchi wa Kilosa na kuwataka kutimiza wajibu,kujiajiri na kuthamini chama cha Mapinduzi.

ZIARA YA KATIBU MKUU CC TAIFA MKOANI MOROGORO KWA UFUPI

NAPE ATOA MAJIBU YA KERO ZA WANANCHI ULANGA

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akizungumza na wananchi wa tarafa ya Mtimbira wilaya ya Ulanga mkoa wa Morogoro.

Nape Nnauye akiongea na wakazi wa kata ya  Karangakero,tarafa ya Mtimbira wilaya ya Ulanga.

Katibu wa CCM,Sixtus Mapunda akihutubia wananchi wa tarafa ya Mtimbira, kwenye viwanja vya shule ya msingi ya Mtimbira .

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi ,Nape Nnauye akihutubia wakazi wa tarafa ya Mtimbira, wilaya ya Ulanga,tarehe 15 April 2013.

ZIARA YA KINANA ULANGA, MOROGORO‏

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi kadi kwa Magdalena Mashinga, alimkabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya kwenye tawi la CCM la Mawasiliano, wilayani Ulanga,Aprili 15, 2013, akiwa katika ziara ya kuimarisha uhai wa chama mkoani Morogoro. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib na Mwenyekiti wa CCM mkoa hu, Innocent Edward. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimsikiliza kwa makini Katibu wa tawi la CCM  Kiwanjani, Ulanga,mkoani Morogoro,  Francis Kanyali aliyekuwa akisoma taarifa, Kinana alipotemebea tawi hilo kukagua uhai wa Chama, Aprili 15, 2013. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib akikagua daftari la wanachama wa CCM kwenye tawi la Mawasiliano, Ulanga mkoani Morogoro, alipofika hapo na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, Aprili 15, 2013. (Picha na Bashir Nkoromo).

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana  akiwa katika picha ya pamoja na  viongozi wa CCM tawi la Ulanga Mjini mkoani Morogoro, baada ya kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo, Aprili 15, 2013. (Picha na Bashir Nkoromo).

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akimpokea Pancras Mogela aliyekuwa mwanachama wa Chadema akipoamua kujiunbga na CCM, Kinana alipotembelea tawi la CCM Viwanjani, Ulanga mkoani Morogoro, kukagua uhai wa Chama kwenye tawi hilo, Aprili 15, 2013. Kushoto ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Muhammed Seif Khatib. (Picha na Bashir Nkoromo).

Kinana akipokea kadi ya mwanachama mpya kutoka Chadema, Kijiji cha Mwaya.

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akikabidhi Mbuzi kwa Nahodha wa timu ya Libenenga, Steven Maundu, baada ya timu hiyo kuibuka mshindi kwa kuibugiza timu ya Nkongo mabao 2-0, katika mechi ya fainali ya Kinana CUP, kwenye Uwanja wa Mwaya, Ulanga mkoani Morogoro, Aprili 15, 2013. Pamoja na zawadi hiyo, ameipatia timu hiyo zawadi ya sh. 100,000 kiasi kinacholingana na alichoipa timu iliyofungwa. Kulia ni  Nahodha wa timu ya Nkongo, Abdallah Mazengo. (Picha na Bashir Nkoromo).

MKUTANO WA CCM KILOSA WAFANA


Katibu wa CCM mkoa  wa Morogoro akihutubia wananchi wa  Ruaha wilaya wa Kilosa.

Mwenyekiti wa  CCM wilaya wa Kilosa  ,Nassoro Udelele akijibu swala la wahanga wa ardhi katika wilaya ya Kilosa,kata ya Ruaha.

Mshairi maarufu wa Morogoro,,Ndugu Maulid Chambilila akighani wakati wa mkutano wa hadhara uiofanyika kata ya Ruaha,wilaya ya Kilosa.

Dk.Mohamed Seif Khatib akihutubia wananchi wa wilaya ya Kilosa ,kata ya Ruaha ambapo aligusia umuhimu wa Muungano.

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi,Nape Nnauye akihutubia wananchi wa wilaya ya Kilosa,kata ya Ruaha na kuwashukuru kufanikisha uchaguzi wa wajumbe wa mabaraza ya katiba.

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu abdulrahaman Kinana  akizungumza na wananchi wa Ruaha wilaya ya Kilosa.

KATIBU MKUU WA CCM,AWASILI MOROGORO LEO

Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahaman Kinana akisalimia wananchi wa Morogoro mara baada ya kuwasili Mkoani hapo,katika makao makuu ya CCM Morogoro.

Katibu Mkuu,Ndugu Abdulrahaman Kinana akiwasalimu wananchi wa Mkoa wa Morogoro,ambapoa atakuwa na ziara ya kikazi mkoani hapo kwa muda wa wiki moja.