FLASH


Monday, January 28, 2013

HONGERA KOMREDI NA KADA KATA YA KAWE JAMES ROCKY MWAKIBINGA KWA KUONESHA NJIA vijana tuige mfano huu



MSHINDI WA LIGI YA KLABU BINGWA VIJANA KAWE CUP'NI NYARA FC TOKA MTAA WA MZIMUNI AMEKABIDHIWA KOMBE NA NG'OMBE,HUKU COCOZ MSHINDI WA PILI AKIJINYAKULIA ZAWADI YA MBUZI NA JEZI.>> — with Stephen Masele

CCM TAWI LA MZUMBE TUNATOA POLE KWA  WANACHAMA WENZETU NA WANANCHI WOTE WALIOCHOMEWA MALI PAMOJA NA NYUMBA ZAO HUKO MTWARA POLE KWA 

Waheshimiwa Hawa Ghasia (Waziri, TAMISEMI) na ya Mohamed Sinani (Mwenyekiti wa CCM Mkoa) zilizopo mtaa wa Sinani.

MTAZAMO WA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA KUHUSU VURUGU ZA MTWARA

MTAZAMO WA KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI CCM TAIFA
NAPE NNAUYE KAHUSU VURUGU ZA MTWARA



Nimefuatilia kwa umakini na kuona kuwa Wakazi wa Mtwara na Lindi wanazo hoja za msingi juu ya suala la gesi, hoja ambazo ni muhimu kusikilizwa na kupatiwa majibu sahihi..! Lakini nyuma ya hoja hizo muhimu kwa wana kusini, KUNA WAHUNI, WAHALIFU AMBAO WAMEDANDIA NYUMA YA HOJA NA KUANZISHA VURUGU, KUCHOMA MALI NA KUHARIBU VITU, Vitendo hivi vya uvunjaji wa Sheria kimsingi havina uhusiano wa moja kwa moja na hoja za gesi.
 
Sisi kama chama tutaendelea kutetea, kutangaza na kulinda haki za kila mmoja. Dhamira hii inatokana na Katiba yetu lakini pia inatokana na sera zetu ambazo zinaunda mazingira ya amani na utulivu katika jamii. Tutaendelea kupiga vita Ubaguzi wa aina zote, Ukabila, Udini, Rangi, Jinsia na wa Majimbo., ili kujenga na kuimarisha Umoja wa Kitaifa.
 
Nasisitiza kuwa “HOJA HALISI” za wanamtwara juu ya gesi isikilizwe na kupewa majibu sahihi, lakini Serikali iwashughulikie wahalifu wote ambao wanataka kutumia Suala hili kama kichaka cha kuendeleza Uharifu na kuvuruga Amani katika nchi.!!. Ni lazima kusisitiza Utawala unaoheshimu sheria lakini pia kusisitiza juu ya Utii wa sheria bila shuruti na kuimarisha Uhusiano baina ya vyombo vya dola na jamii.
Kauli za baadhi ya viongozi na watu wa kawaida zinaonesha wazi hawana Dondoo sahihi juu ya Suala hili, kauli na matendo yao vinaashiria mtengano, na kukuza uhasama. Nitoe wito kwa kundi hili, kuona sababu ya kuifuatilia na kuielewa hoja halisi ya wanamtwara juu ya gesi, ambayo haisisitizi kujitenga na wala haina asili ya choyo. Lakini baada ya kuielewa, wasaidie wengine pia kuielewa hoja halisi ya wana-mtwara inayohoji juu ya maslahi. Ni imani yangu kuwa tutashirikia pamoja katika Kuimarisha Udugu na Umoja wa kitaifa, na kuwa msitari wa mbele katika kulinda, kutunza na kusimamia Amani na Utulivu wetu kama taifa.
 
Chanzo www.facebook.com/Nape Nnauye