FLASH


Wednesday, November 13, 2013

ZIARA YA RAIS KIKWETE KWA UFUPI KATIKA MIKOA YA KAGERA NA GEITA

JK AZINDUA SHULE YA MWEKEZAJI MZALENDO SEKTA YA MADINI.


 Rais Jakaya Kikwete amezindua shule ya msingi ya Ng'anzo iliyojengwa na mwekezaji mzalendo wa sekta ya madini (dhahabu) Emmanuel Gungu ambaye ni mmiliki na Mkurugenzi wa Kampuni ya NGASALI LTD.
 Shule hii imegharimu kiasi cha shilingi milioni 460 hadi kukamilika kwake ina vyumba saba vya madarasa ya kisasa, jengo kubwa la utawala, maktaba moja, nyumba saba za walimu, matundu manne ya vyoo vya walimu, matundu 24 ya vyoo kwaajili ya wanafunzi na thamani za ofisi na madawati.
 Rais JK amewataka wawekezaji kuwa na moyo wa kuwekeza na kuisaidia jamii kwa kuzisogeza karibu huduma muhimu.
 Wanafunzi toka shule mbalimbali  wakiwa na wazazi wao na wananchi wengine wamejumuika hapa kushuhudia uzinduzi huu wa shule ambao umefanyika katika kijiji cha ng'anzo mji wa Ushirombo wilaya ya Bukombe mkoani Geita.
 Aidha Rais amempongeza mkurugenzi huyo kwa kuanzisha pia ushirika wa wachimbaji wadogowadogo wa dhahabu ambao kwa kipindi kifupi umefanikiwa kuwa na hisa za milioni 3.2 ambapo kila mwanachama hununua hisa tano kwa shilingi 25,000/= kwa kila hisa.

JK ameuchangia ushirika huo kiasi cha shilingi milioni 2 huku akiahidi kuendelea kuwapatia wachimbaji wadogo maeneo ya uchimbaji ikiwemo vifaa vya kisasa.

Naye Naibu Waziri wa NIshati na Madini Steven Masele ameahidi kupeleka umeme kwenye maeneo yote ya wachimbaji wadogo wa dhahabu na almasi ili kuwaongezea uwezo na ufanisi kupitia vifaa vya umeme kuchenjulia na kusaga mawe yenye madini.
Kusanyiko na mazingira ya shule ya msingi ya Ng'anzo iliyojengwa na mwekezaji mzalendo wa sekta ya madini (dhahabu) Emmanuel Gungu ambaye ni mmiliki na mkurugenzi wa kampuni ya NSAGALI LTD.