FLASH


Wednesday, February 17, 2016

SHUKRANI



                                                       
YAH:SHUKRANI YA UFANIKISHAJI MKUTANO WA WANACHAMA TAWI MAALUM MZUMBE TAREHE 14/02/2016
 Ndugu wanachama wa chama cha mapinduzi, nimatumaini yangu sote tu wazima wa afya kwa uwezo wake muumba. Kama ambayo kichwa cha habari hii hapo juu kinavyojieleza ni kwamba siku ya tarehe 14/02/2016 uongozi wa ccm tawi maalum chuo kikuu mzumbe morogoro tulifanikiwa kuendesha mkutano wa tawi uliotukutanisha wanachama wa ccm tawi maalum mzumbe pamoja na viongozi wa jumuiya zingine zilizo chini ya chama cha mapinduzi ambazo ni jumuiya ya wazazi, jumuiya ya vijana wa ccm na umoja wa wanawake Tanzania. Mkutano huu ulifanikiwa kwa kiasi kikubwa lakini kama tujuavyo shughuli yoyote ni watu hivyo namaanisha ufanisi wa mkutano huu pia ulitokana na ushiriki wa watu kwa hali na mali kwa kiasi kikubwa hivyo nawiwa kutuma salamu zangu za shukrani kwa wote waliofanikisha mkutano huu ukafanyika.
Shukrani za dhati kabisa zimwendee Mh, diwani wa kata ya mvomero Bi. Recho Kingu kwa kukubali kuacha majukumu yake na kukubali kuja kuwa mgeni rasimi katika mkutano huo mbali  na kuwa mgeni rasimi Mh. Kingu pia alishirikiana nasi kwa ukaribu mkubwa kuhakikisha mkutano huu unafanyika kama ilivyokusudiwa.
Bila kumusahau Mh. Murad mbunge wa jimbo la mvomero naye hakuwa nyuma katika kuhakikisha mkutano huu unafanyika bila kuwa na kipingamizi chochote aidha tawi maalum mzumbe tunathamini sana mchango wake na kwa niaba ya wanachama wote niseme asante sana mh. Mbunge wetu kwa ushiriki wako katika kuwezesha mkutano huo ukawa wa mafanikio.
Nichukue fursa hii pia kuwashukru Ndugu Boniphace Maiga na Maliki Malupu kwa kujitolea kutoa darasa la itikadi na hamasa kwa wajumbe waliohudhuria mkutano huo naamini wajumbe walijifunza mengi kutoka kwa wazungumzaji pia walihamasika vilivyo.
Napenda pia kumshukru rais wa serikali ya wanafunzi wa mzumbe Mh. Yona Habiye kwa ushiriki wake wa hali na mali kuhakikisha mkutano wetu unafanikiwa. Lakini pia niwashukru viongozi wa shirikisho mkoa wa morogoro wakiongozwa na comrade Kimako kwa kuja kujumuika nasi na kutoa ufafanuzi kwa wajumbe juu ya changamoto zinazotukabili kama wanachama wa shirikisho mkoa wa morogoro, bila kumusahau ndugu Alferd Salwa rais mstaafu wa serikali ya wanafunzi chuo kikuu mzumbe kwa sapoti yake katika kufanikisha mkutano.
Mwisho kabisa niwashukru viongozi wote wa tawi maalum chuo kikuu mzumbe kwa ushirikiano wetu tumeonesha kwa vitendo dhana ya UMOJA NI USHINDI na niwashukru pia wanachama wote waliojitokeaza kushiriki katika mkutano huo nizidi kuwaomba kwamba tusiwe wazungumzaji tu bali tuwe watendaji ili tumusapoti Rais wetu Dr, John Magufuli katika kutimiza ahadi zake kwa watanzania maana jukumu la kutekeleza ilana ya uchaguzi ya ccm 2015/2020 ni jukumu la kila mwana ccm kwa nafasi aliyo nayo katika jamii yake.
Asanteni sana wanachama wote wa tawi maalum chuo kikuu mzumbe na wote tulioshiriki katika mkutano huo.
“SASA KAZI KUJENGA NCHI NA KUKIJENGA CHAMA CHETU”  
#KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Imetolewa na:-
Katibu ccm tawi maalum chuo kikuu mzumbe
                                                               Gwodwin Komba
                                                                    15/02/2016