FLASH


Wednesday, February 6, 2013

KUTOKA KIGOMA KWA UFUPI

WA CCM RAIS KIKWETE AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO YA MIAKA 36 YA CCM MJINI KIGOMA LEO

Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Kikwete akiongoza matembezi ya maadhimisho ya miaka 36 ya CCM, leo asubuhi kutoka eneo la Mnarani hadi ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma leo. Wengine ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip Mangula, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kigoma Dk. Amani Kaborou, Mama Salma Kikwete, Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Katibu wa NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Dk. Asha-Rose Migiro (kulia)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya mshikamano ya Miaka 36 ya CCM, mjini Kigoma leo
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiongoza matembezi ya Mshikamano ya Maadhimisho ya Miaka 36 ya CCM mjini Kigoma leo
Matembezi hayo yakipita eneo la Burega, Barabara ya Kigoma-Ujiji
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi CCM, Nape Nnauye akiwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM, Sadifa Abdalla na Mkuu wa wilaya ya Kigoma Jumanne Maneo
Wananchi wakishangilia wakati matembezi yakipita barabara ya Ujiji Kigoma kwenda Ofisi ya CCM ya mkoa wa Kigoma leo
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akimsalimia Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana baada ya kuwasili eneo la Mnarani mjini Kigoma tayari kwa matembezi hayo. Wapili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara), Philip Mangula na wengine ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM (Bara) Mwigulu Nchemba na Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Dk. Asha-Rose Migiro
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiwapungia mkono wananchi msafara wa matembezi hayo ulipokaribika kufika Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
Rais Kikwete akiwa na Nape na Kinana baada ya msafara wa matembezi hayo kuwasili
 Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikweye akiwa na muaasisi mmoja wa CCM ( ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) baada ya matembezi kufika Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
 
 Mama Salma Kikwete akisalimia baada ya msafara wamatembezi hayo kufika Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma
Mwenyekiti wa CCM, Rais Kikwete na msafara wake wakiwa wameketi meza kuu Ofisi ya CCM mkoa wa Kigoma baada ya matembezi hayo.
"NDUGU WANANCHI, NAWAPONGEZA KWA KUSHIRIKI KWA WINGI KWENYE MATEMBEZI HAYA. HAPA SISEMI MENGI TUKUTANE MCHANA PALE UWANJA WA LAKE TANGANYIKA" Akasema Rais Kikwete wakati akizungumza na wananchi baada ya matembezi hayo. (PICHA ZOTE NA BASHIR NKOROMO@Daily Nkoromo Blog)