FLASH


Friday, February 8, 2013

CCM NA MIAKA 36

MAMA SALMA  KIKWETE NA MBUNGE WA MTAMA BENARD MEMBE KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 36 YA CCM


IMG_6755
 
  Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa mkoa wa Lindi waliohudhuria sharehe za kutimiza miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Rondo kata ya Chiponda mkoani Lindi tarehe 5.2.2013.
IMG_6468 
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akifungua rasmi  jengo la CCM  Tawi la Rondo kata ya Chiponda huko Lindi Vijijini wakati wa kilele cha sherehe ya kutimiza miaka 36 ya CCM zilizofanyika  kimkoa kijijii hapo tarehe 5.2.2013. Kulia kwa Mama Salma ni Mjumbe wa NEC Taifa, Mbunge wa Mtama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe.
IMG_6475 
Mke wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akifurahia mara baada  ya kulifungua rasmi  jengo la CCM  Tawi la Rondo kata ya Chiponda huko Lindi Vijijini wakati wa kilele cha sherehe ya kutimiza miaka 36 ya CCM zilizofanyika  kimkoa kijijii hapo tarehe 5.2.2013. Kulia kwa Mama Salma ni Mjumbe wa NEC Taifa, Mbunge wa Mtama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe.
IMG_6544 
Ngoma ya Linyamwa ya kabila la Wamwera ikichezwa na wananchi wa kijiji cha Mpenda kutoka  wilaya ya Lindi vijijini wakati wa kilele cha sherehe ya kutimiza miaka 36 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi zilizoazimishwa kimkoa katika kijiji cha Rondo tarehe 5.2.2013.
IMG_6572 
Mama Salma Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe za kutimiza miaka 36 ya CCM Mkoani Lindi akijumuika na wacheza ngoma ya Linyamwa kucheza ngoma hiyo. Sherehe hizo zilifanyika katika kijiji cha Rondo huko Lindi vijijini tarehe 5.2.2013.
IMG_6685 
Mjumbe wa NEC na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard  Membe akimvisha skafu Bwana Omary Issa kutoka Chama cha Wananchi, CUF,  akiwa ni miongoni mwa  wanachama wapya waliojiunga na CCM kutoka vyama vingine vya siasa wakati wa kilele cha sherehe za kutimiza miaka 36 ya kuzaliwa chama hicho.
IMG_6702 
Mjumbe wa NEC Taifa kutoka wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akimkabidhi kadi ya CCM mwanachama mpya ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja wakati wa sherehe za kutimiza miaka 36 ya chama hicho zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Rondo huko Lindi Vijini tarehe 5.2.2013,
IMG_6746 
Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba kutoka kwa mgeni rasmi Mama Salma Kikwete wakati wa kilele cha kutimiza miaka 36 ya ChamaCha Mapinduzi.  Sherehe zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Rondo kata ya Chiponda huko Lindi vijijini tarehe 5.2.2013.