MAMA SALMA KIKWETE NA MBUNGE WA MTAMA BENARD MEMBE KATIKA SHEREHE ZA MIAKA 36 YA CCM
Kikwete akihutubia mamia ya wananchi wa mkoa wa Lindi
waliohudhuria sharehe za kutimiza miaka 36 ya Chama cha Mapinduzi
zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Rondo kata ya Chiponda mkoani
Lindi tarehe 5.2.2013.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akifungua
rasmi jengo la CCM Tawi la Rondo kata ya Chiponda huko Lindi Vijijini
wakati wa kilele cha sherehe ya kutimiza miaka 36 ya CCM zilizofanyika
kimkoa kijijii hapo tarehe 5.2.2013. Kulia kwa Mama Salma ni Mjumbe wa
NEC Taifa, Mbunge wa Mtama na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe.
Mke
wa Rais na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) wa wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete akifurahia
mara baada ya kulifungua rasmi jengo la CCM Tawi la Rondo kata ya
Chiponda huko Lindi Vijijini wakati wa kilele cha sherehe ya kutimiza
miaka 36 ya CCM zilizofanyika kimkoa kijijii hapo tarehe 5.2.2013.
Kulia kwa Mama Salma ni Mjumbe wa NEC Taifa, Mbunge wa Mtama na Waziri
wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa Bernard Membe.
Ngoma
ya Linyamwa ya kabila la Wamwera ikichezwa na wananchi wa kijiji cha
Mpenda kutoka wilaya ya Lindi vijijini wakati wa kilele cha sherehe ya
kutimiza miaka 36 ya kuzaliwa Chama Cha Mapinduzi zilizoazimishwa kimkoa
katika kijiji cha Rondo tarehe 5.2.2013.
Mama
Salma Kikwete aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe za kutimiza miaka 36
ya CCM Mkoani Lindi akijumuika na wacheza ngoma ya Linyamwa kucheza
ngoma hiyo. Sherehe hizo zilifanyika katika kijiji cha Rondo huko Lindi
vijijini tarehe 5.2.2013.
Mjumbe
wa NEC na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mheshimiwa
Bernard Membe akimvisha skafu Bwana Omary Issa kutoka Chama cha
Wananchi, CUF, akiwa ni miongoni mwa wanachama wapya waliojiunga na
CCM kutoka vyama vingine vya siasa wakati wa kilele cha sherehe za
kutimiza miaka 36 ya kuzaliwa chama hicho.
Mjumbe
wa NEC Taifa kutoka wilaya ya Lindi Mjini Mama Salma Kikwete
akimkabidhi kadi ya CCM mwanachama mpya ambaye jina lake halikuweza
kufahamika mara moja wakati wa sherehe za kutimiza miaka 36 ya chama
hicho zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Rondo huko Lindi Vijini
tarehe 5.2.2013,
Baadhi
ya wananchi wakisikiliza kwa makini hotuba kutoka kwa mgeni rasmi Mama
Salma Kikwete wakati wa kilele cha kutimiza miaka 36 ya ChamaCha
Mapinduzi. Sherehe zilizofanyika kimkoa katika kijiji cha Rondo kata ya
Chiponda huko Lindi vijijini tarehe 5.2.2013.
No comments:
Post a Comment