CCM YAWASHA MOTO LEO GAIRO,
KINANA |
GAIRO, MOROGORO, Tanzania
Chama Cha Mapinduzi (CCM) leo kinatarajiwa 'kuuteka' mji wa Gairo
kitakapofanya mkutano mkubwa wa hadhara kuanzia saa kumi jioni katika
mji huo.
Kulingana na shamrashamra na simulizi zilizvyotanda miongoni mwa
wananchi katika maeneo mbalimbali hapa Gairo, mkutano huo unatarajiwa
kuhudhuriwa na maelfu ya watu, kwa ajili ya kumshudia Katibu Mkuu wa
CCM, Abdulrahman Kinana ambaye anakuwa Gairo kwa mara ya kwanza tangu
kuteuliwa kwake kushika wadhafa huo.
Mbali na Kinana ambaye aliwasili jana jioni, akitokea Kilosa, viongozi
wengine wanaotarajiwa kuwasha moto kwenye mkutano huo,ni Katibu wa
Halmashauri Kuu ya Taifa, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Katibu wa
NEC, Oganaizesheni, Dk. Mohammed Seif Khatib.
Kabla ya mkutano huo Kinana na ujumbe wake wamepangiwa kufanya shughuli
mbalimbali za ujenzi wa Chama na ukaguzi wa ilani ya CCM, ikiwa ni
pamoja na Kinana kufanya kikao cha ndani na mabalozi na viongozi wa
Chama ngazi wa kata zioizopo karibu na makao makuu ya wiyala.
CCM YAFUNIKA KILOSA, MAMIA WAJITOKEZA KUMSIKILIA KINANA
Katibu Mkuu wa CCM,Abdulrahman Kinana (kulia) akihutubia mkutano mkubwa wa hadhara leo jioni mjini Kilosa, mkoani Morogoro.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akisaini cha kitabu cha wageni
kwenye Shina la wajasiriamali wakereketwa wa CCM la Dinima, Kilosa
katika ya kuwasili mjini Kilosa mkoani Morogoro kuhutubia mkutano mkubwa
wa hadhara leo Aprili 17, 2-13.Vijana wakisahngilia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, wakati msafara huo ukitoka Ifakara kwenda Kilosa leo
Katibu Mkuu wa CCM, Kinana akizungumza na wanachama wa CCM shila namba 15, tawi la CCM Mbuni B, Kilosa. Kushoto ni Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi. Alyevaa miwani (kulia) ni Katibu wa NEC, Oganaizesheni, Dk. mhammed Seif Khatib.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nap Nnauye (kushoto) akimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana (kulia) wakati amekaa na wajumbe wa shina namba 15, tawi la CCM Mbuni B.
Viongozi kuanzia ngazi za mashina wa CCM katika wilaya ya Kilosa, wakizungumza na Kinana kwenye ukumbi wa Comfort, wilayani humo
Katibu wa NEC, Oganaizesheni Mohamed Sif Khatib akitazama mahidi yalivyostawi kwenye shamba la mkulima maarufu wa wilayani Kilosa
NAPE AWASHUKIA WANASIASA KANJANJA
Wanachama wa CCM wakiwa kwenye mkutano wa ndani na Katibu Mkuu wa CCM Taifa,Ndugu Abdulrahaman Kinana. |
Wazee waasisi na wanachama hai wa Chama Cha Mapinduzi wakimsikiliza Katibu Mkuu,kwenye mkutano wa ndani hapo Kilosa. |
Katibu wa NEC,Oganizesheni, Dr. Mohamed Seif Khatibu akisalimia wananchi wa Kilosa. |
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi akihutubia wananchi wa Kilosa na kuwapa pongezi kushiriki kwenye mchakato wa Katiba Mpya, na pia aliwagusia wananchi kuwa makini na makanjanja wa kisiasa. |
Katibu Mkuu wa CCM akihutubia wananchi wa Kilosa na kuwataka kutimiza wajibu,kujiajiri na kuthamini chama cha Mapinduzi. |
No comments:
Post a Comment