FLASH


Friday, April 5, 2013

UMOJA NI USHINDI KILA RAHELI NAPE

 KATIBU WA ITIKADI NA UENEZI TAIFA NAPE NAUYE ATINGA MKOANI KILIMANJARO LEO KUUNGURUMA MOSHI KESHO 


 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye akilakiwa na Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro, Iddi Mohammed baada ya kuwasilili jioni hii kwenye Ofisi ya CCM mkoa huo mjini Moshi. Kesho Nape anatarajiwa kufungua semina ya Halmashauri Kuu ya Mkoa huo ya CCM na baadaye kuhutubia mkutano mkubwa wa hadhara mjini Moshi.
 Katibu wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Steven Kazidi (wapili kushoto) akimtambulisha Mwenyekiti wa UVCCM mkoa huo, Frederick Mushi kwa Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi. Kulia ni Mwenyekiti wa CCM Moshi Mjini Elizabeth Minde.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akivishwa skafu na Kijana wa CCM baada ya kuwasili Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanajro mjini Moshi jioni hii.
 Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akishiriki kucharaza ngoma, iliyokuwa inapigwa na kundi la sanaa la CCM, baada ya kuwasili kwenye Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro jini Moshi jioni hii.
 Katika ziara hiyo Nape ameambatana na Vijana waliojiengua hivi karibu kutoka Chadema, Mtela Mwampanga na aliyekuwa Naibu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema, Juliana Shonza. Pichani, Mwampamba na Shonza wakisalimiana na vijana wenzao ambao pia wamehamia CCm hivi karibuni kutoka Chadema mkoani Kilimanjaro, David Waryoba (kushoto) na Yona Makwaya (wapili kushoto)
Vijana wakimsubiri Nape kwa shauku alipowasili Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi jioni hii.
Nape akitia saini kwenye kitabu cha wageni, katika Ofisi ya CCM mkoa wa Kilimanjaro mjini Moshi jioni hii. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kilimanjaro Iddi Mohammed.(Picha zote na Bashir Nkoromo)

No comments:

Post a Comment