FLASH


Friday, April 5, 2013

PAMOJA NAKUAMUA KUTAFUTA UFUMBUZI CCM TUWE MAKINI KWENYE VYUO NA MATAMKO

CCM yaunda kamati kushughulikia mgogoro

                                     Naibu Katibu Mkuu Bara, Mwigulu Nchemba. 
0
Arusha. Chama Cha Mapinduzi (CCM) hatimaye kimeingilia kati mgogoro wa ardhi Loliondo, baada ya kuunda kamati maalumu kuchunguza mgogoro huo, itakayoongozwa na Naibu Katibu Mkuu Bara, Mwigulu Nchemba.

Wakati chama hicho kikichukua hatua hiyo, wanafunzi kutoka Wilaya ya Ngorongoro wanaosoma vyuo mbalimbali mkoani Arusha, wametangaza nia ya kuacha masomo warejee vijijini kutetea ardhi ya wazee wao.

Akizungumza mjini hapa juzi, Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Ngorongoro, Abraham Sakay alisema kutokana na mgogoro huo, waliamua kwenda kuonana na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Sakay alisema CCM Ngorongoro, inaungana na wanachama kuipinga Serikali, kutwaa ardhi ya vijiji kilomita za mraba 1,500, lakini imeona siyo busara sasa viongozi wote wa kuchaguliwa ambao ni wa CCM kujiuzulu.

Viongozi wote wa kuchaguliwa katika wilaya hiyo, ambao wanatishia kujiuzulu wanatoka CCM.Sakay alisema viongozi wa kitaifa wa CCM, wanatarajiwa kufika wilayani humo mapema iwezekanavyo kuzungumza na viongozi wa wilaya na wanachama wa CCM.

Hata hivyo, wakati CCM ikiingilia kati mgogoro huo, juzi zaidi ya wanachama 200 wa CCM, walitupa kadi baada ya mkutano uliofanyika jirani na Uwanja wa Ndege Loliondo.
Akizungumza juzi, Mwenyekiti wa wanafunzi hao, Albert Selembo alisema vijana wanaotoka wilayani Ngorongoro wamesikitishwa na uamuzi wa Serikali.

Naye Katibu wa Umoja huo, Flavian Massango anayesoma Chuo Kikuu cha Makumira Arusha, alisema iwapo Serikali ya CCM ina mpango wa kutumia uhifadhi kwa kulaghai ardhi, hautafanikiwa.

Alisema wakiwa wanazuoni wanaunga mkono maazimio yaliyotolewa na Baraza la Malaigwanani (viongozi wa mila) na viongozi wa siasa ya kutoitambua Kampuni ya Uwekezaji ya Ottler Business Corporation

No comments:

Post a Comment